
Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa kesho Jumatano 21/11/2018 umesogezwa mbele na sasa utachezwa siku ya Ijumaa 23/11/2018.
Mabadiliko hayo yamefanywa ili kuwapa nafasi wachezaji wetu waliokuwa kwenye timu zao za Taifa kujiunga na kikosi chetu ili kuwa sehemu ya wachezaji ambao watacheza mchezo huo.
Ukaichana na wachezaji hao, Simba itamkosa beki wake wa kulia Shomari kapombe ambaye ameumia akiwa kambini na timu ya taifa 'Taifa Stars'.
Tayari Kapombe ameshaanza kufanyiwa matibabu huko Afrika Kusini ili kurejea katika hali yake ya kawaida hapo baadaye.