Tunafahamu kwamba Zanzibar inahistoria kubwa juu ya ugonjwa wa kipindupindu ambao husababishwa na uchafu wa mazingira, pamoja na kutokuwa na uwangalizi katika uhifadhi wa taka zetu.
Niukweli ulio wazi kuwa Serikali kwa kushirikiana na Mabaraza ya Manispaa ya Zanzibar wameweza kupiga hatua katika harakati za kutunza mji wa Zanzibar pamoja na vitongoji vyake ikiwemo kufanywa usafi katika maeneo mbalimbali, kuwekwa madebe na makontena ya kuhifadhia taka katika mitaa mbalimbali na kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya kutunza mazingira na matumizi ya vyoo katika majumba yao.
Zipo sehemu hapa Zanzibar bado kuna baadhi ya wananchi hawana utamaduni wa kuyatumia makontena katika kuhifadhia taka zao na kuamua kwa makusudi kumwaga takataka na uchafu sehemu yeyote wanapoamua na wapo wengine wanayatumia vyema makontena na madebe ya kuhifadhia taka hadi kujaa na kuzimwagia chini ya kontena.
Wananchi wa Kwamtipura Shehia ya Kivumbi walia na hali ya uchafu pamoja na harufu mbaya za taka zilizohifadhiwa kwenye makontena katika maeneo yao ambazo huchelewa kuja kuchukulia na Baraza LA Manispaa ili kwenda kutupwa sehemu husika jambo linalowatia hofu usalama wa afya zao.
Mwandishi wa Zanzibar 24 ameshuhudia taka zilivyojaa katika kontena hadi kumwagika chini na kutoa harufu mbaya huku watoto wakicheza karibu na kontena hilo lililokaribu na makaazi ya watu hali ambayo inatia hofu ya kutokea kwa maradhi ya mripuko ikiwemo matumbo ya kuharisha na kipindupindu.
Ushauri ni jambo zuri, Tunawaomba Mamlaka husika msisubiri kuitwa muwe mnakagua makontena ya taka Mara kwa Mara ili kuondoa kero hizi za kila siku na baadae kuwabebesha lawama wananchi kwa madai hawakubaliani na jukumu la kusafisha mazingira yao.
Zipo baadhi ya sehemu asubuhi na jioni mnakwenda kuchukua taka hasa katika maeneo ya mjini mfano darajani na maeneo mengine ya karibu na mji lakini maeneo ya N’gambu mnajisahau hadi wiki ndio mnapita jambo ambalo kiutendaji mnakosa ufanisi.
Amina Omar.