Rais
Mstaafu Benjamin Mkapa akihutubia wakati akiongoza harambee ya
kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) katika hafla
iliyofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana usiku.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akihutubia katika harambee hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi,Bw. Godfrey Simbeye akihutubia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akihutubia.
Wadau wakiwa kwenye harambee hiyo.
Makofi
yakipigwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa,
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi, Bw.
Godfrey Simbeye na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita
Gold Mine (GGM), Bw. Tenga B. Tenga.
Wadau wakiwa kwenye harambee hiyo.
Harambee ikiendelea.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akitoa zawadi ya picha iliyonunuliwa kwa sh. milioni moja katika harambee hiyo.
Rais Mkapa akimkabidhi picha Salama Mussa kutoka Benki ya NBC baada ya kuinunua katika harambee hiyo. Kulia ni Waziri Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama na
wa pili kushoto ni Mdau Teddy Mapunda mratibu wa harambee hiyo.
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez baada ya kuinunua katika harambee hiyo.
Rais
Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha ya simba Mkurugenzi wa Mauzo
na Masoko wa Hoteli ya Serena, Bw. Seraphin Lusala baada ya kuinunua
kwenye harambee hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM),
Bw. Tenga B. Tenga akimkabidhi Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa mfano wa
hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 zilizo tolewa na mgodi huo
kuchangia mfuko huo.
Na Dotto Mwaibale
RAIS Mstaafu
Benjamin Mkapa amewataka wadau mbalimbali na wananchi kuendelea
kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwa ajili ya
kukabiliana na ugonjwa huo nchini ambapo zaidi ya sh.milioni 200
zilipatikana.
Mkapa
alitoa ombi hilo wakati akiongoza harambee ya kuchangia mfuko huo
iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa
na viongozi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya nje na ndani pamoja
na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
"Ni
wajibu kwa kila mwananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia mfuko
huu ili kusaidia mapambano ya Ukimwi hapa nchini na kuwa mapmbano hayo
si ya mtu mmoja" alisema Mkapa.
Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mkapa ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha za Ukimwi katika bajeti zake.
Akizungumza katika harambee hiyo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema kwamba Serikali itaendelea kusimamia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika matumizi ya fedha hizo.
Mhagama
alisema asilimia 60 ya fedha hizo zitatumika kununulia madawa, asilimia
25 itatumika katika kutoa huduma za kinga pamoja na kutoa elimu ya
kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi na asilimia 15 zitatumika kwa
ajili ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa programu za Ukimwi.
Mhagama
aliongeza kuwa matumizi ya dawa za kufubaza VVU kwa wanawake ni
asilimia 92.9 wakati wanaume ni 86.1 na kuwa katika tisini ya tatu kati
ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15-64 ambao wametoa taarifa
kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU asilimia 87.7 ya watu hao
inaonyesha kiasi cha VVU kimefubazwa wanawake ni asilimia 89.2 na
wanaume ni asilimia 84.
Alisema
utafiti huo pia umeonyesha kuwa maambukizo mapya ya VVU (HIV incidence)
kwa mwaka kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 Tanzania Bara ni asilimia
0.29 ambayo ni sawa na watu 81,000.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko huo, Bw. Godfrey Simbeye alisema sekta binafsi imeunga
mkono kwa kiasi kikubwa katika kuchangia mfuko huo na kuwa hakutakuwa
na matumizi mabaya ya fedha hizo na zitakwenda kutumika kwa kile
kilichokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS),
Dk. Leonard Maboko alimshukuru Rais Mstaafu Mkapa kwa kukubali
kushiriki kuongoza harambee hiyo na kueleza kuwa Tacaids imekuwa
ikiendesha harambee mbalimbali pamoja na kuandaa mashindano ya michezo
na viingilio vyake vimekuwa vikiingia katika mfuko huo.