Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na Mheshimiwa Yoshida
Masaharu Balozi wa Japan Nchini Tanzania wakisaini kitabu cha wageni
baada ya kuwasili kijiji cha Kasenda kwa ajili ya Makabidhiano ya Mradi
wa Soko la Samaki la Kimataifa na kusaini mkataba wa ukarabati wa
barabara yenye urefu wa Kilometa 1 ya kutoka Mganza kwenda Kasenda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Chato Bw;Joel Hari na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida
Masaharu wakisaini mkataba wa ukarabati wa barabara ya Mganza hadi
Kasenda Kilometa 1 huku wakishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa na
Wilaya ya Chato.
Waziri
wa Nishati (Mb) Medard Kalemani wa kwanza kulia aliyevaa shati jeupe
akijadili jambo pamoja na Mheshimiwa Balozi Yoshida Masaharu, Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita na Bathromeo manunga Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Chato
Balozi
wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu aliyevaa miwani na
tai nyekundu pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato bw;
Joel Hari wakiweka jiwe la makabidhiano ya mradi wa Soko la Kimataifa
la Samaki ambalo limefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa Gharama ya
Shilingi milioni 320 kijiji cha Kasenda Chato.
Balozi
wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu akifurahi na Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel baada ya makabidhiano ya Soko
la Samaki la Kimataifa lililopo kijiji cha Kasenda Kata ya Mganza Wilaya
ya Chato.
Balozi
wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu aliye vaa miwani
na tai nyekundu akiwa na Viongozi wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato
baada ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Soko la Samaki la Kimataifa
la Kasenda Wilayani Chato.Watatu kutoka kushoto kwa balozi ni Waziri wa
Nishati (Mb) Mheshimiwa Medard Kalemani na Shaban Ntarambe Mkuu wa
Wilaya ya Chato na Kulia kwa balozi aliyevaa miwani na suti ya kijivu ni
Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel pamoja na Bw; Joel Hari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato.
Na.Magesa Jumapili. Geita RS
Serikali
ya watu wa Japan imekabidhi mradi wa Soko la Samaki la kimataifa kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato wenye thamani ya shilingi milioni 320 na kusaini
makubaliano ya ukarabati wa barabara ya Mganza - Kasenda ili kurahisisha
usafirishaji wa mazao ya ziwani.
Akizungumza
baada ya kukabidhi mradi huo kwa Serikali Balozi wa Japan nchini Tanzania
Mheshimiwa Yoshida Masaharu amesema mradi huo umetolewa na Serikali ya Japan
kwa watu wa Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa urafiki wa siku nyingi katika
utekelezaji wa miradi ya kilimo na uvuvi.
''Mradi wa huu ulitolewa baada ya
kuona soko la Kasenda liko katika hali mbaya na samaki kuharibika kwa kukosa
miundombinu ya kuhifadhi ndipo Japan ikachukua hatua za haraka kwa kutoa fedha
dola za kimarekani 148,146 kwa ajili ya kujenga soko na kukarabati soko la
zamani''. Utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2017 na sasa wananchi wanaendelea
kunufaika.
Awali
akisoma taarifa ya mradi huo kabla ya makabidhiano mkurugenzi wa Halmashauri ya
Chato Joel Hari amesema mradi unahusisha ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia
samaki na ukarabati wa sokola zamani.Ameeleza kuwa soko lipo chini ya
Halmashauri ya Chato likiwa na wanachama 241 huku likikasimiwa kukusanya
shilingi milioni 140 kwa mwaka huku likitoa huduma kwa nchi za Rwanda,Burundi,
Uganda na Congo DRC.
Kwa
upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru
balozi wa Japan nchini kwa miradi hiyo na kumwomba kuangalia na Wilaya zingine
za Mkoa wa Geita ili nazo zinufaike na miradi ya namna hiyo.
Aidha, ameutaka uongozi wa soko kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Chato kuhakikisha malengo yote yaliyokusudiwa
kwa mradi huo yanatekelezeka na kuleta faida ili watu wote wanaofanya kazi
katika soko hilo waongeze kipato kwa kuwa kazi ya Serikali ya awamu ya tano ni
kujenga miundombinu bora na kuweka mazingira wezeshi ya kusaidia kuendesha
biashara.Mhandisi Robert Gabriel ameahidi kuangalia namna ya kutafuta fedha kwa
ajili ya kujenga vibanda vya pembeni mwa soko ili kuwe na mazingira mazuri ya
kufanya biashara.
Mbunge
wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mheshimiwa Medard Kalemani amemshukuru
Balozi Yoshida kwa kutoa miradi hiyo Wilayani Chato na kuomba pia kusaidia
ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari.
Amewataka wananchi wa Chato na
Kasenda kutumia fursa ya uwepo wa mradi huo kujenga biashara na kutoa wito kwa
wenye mitaji midogo kuitunza ili ikuwe.Katika makabidhiano hayo Serikali ya
Tanzania na Japan zimesaini mkataba wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa
Kilometa 1 kutoka Mganza hadi Kasenda ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za
kutoka ziwani.