Mamlaka za Mapato za Africa Mashiriki zaungana kupambana Rushwa - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, June 02, 2018

Mamlaka za Mapato za Africa Mashiriki zaungana kupambana Rushwa

HABARI KUU

Mamlaka za Mapato za Africa Mashiriki zimesema zitashirikiana katika  kupambana na Vitendo vya Rushwa vinavyojitokeza katika ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia malengo waliyoyakusudia katika kukusanya mapato.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mkutano wa siku mbili uliwashirikisha makamishna wa Mamlaka za mapato za nchi sita,uliofanyika mjini Zanzibar Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Charles kichere amesema ili malengo ya ukusanyaji wa mapato yaweze kufikiwa ni vyema kuandaa mikakati ya kuzuia vitendo vya Rushwa.
Amesema pia wamekusudia kuimarisha tozo kwa wafanya Biashara binafsi na wadogo wadogo ili kuimarisha vyanzo vya upatikanaji wa mapato pamoja na kufuatilia Bidhaa za magendo zinazoingizwa nchini kinyume na uataratibu.
Amesema mamlaka ya mapato imekusudia pia kuandaa sheria ya kuzuia bidhaa mabazo hazina Viwango zinazoingizwa kinyume na sheria ili kuziweka nchi za Africa mashariki kutokuwa na soko la Bidhaa zisizo na viwango ambazo zinakwepa kulipa kodi.
Amesema mpaka sasa kuna mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo katika kipindi cha miezi kumi ilioita ukusanyaji wa mapato umeengezeka kwa asilimia 16 kutoka 14 katika kipindi cha miezi iliopita.
Aidha ametowa wito kwa makamishna wenzake kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kupeana taarifa muhimu za wafanya biashara wanaokwepa kulipa kodi ili waweze kuchuliwa hatua za kisheria.
Kwa Upande wake Kamishna wa Bodi ya mapato Zanzibar ZRB Joseph Abdallah Meza wataendelea kushirikiana na maafisa wa TAR katika Ukusanyaji wa mapato ili kuimarisha maendeleo ya nchi.
Amesema amefurahishwa kwa mkutano huo kufanyika hapa Zanzibar na kuhakikisha wataendelea kusimamia ipasavyo vyanzo vya mapato pamoja na kutowavumilia wafanya biashara wanaokiuka sheria za ingizaji wa biashara zao Nchini.
Kwa Upande wake kamishna msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Ruwanda Abiambele Kajingi amesema watahakisha wanaendelea kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi na wafanya biashara wa ruwanda ili kufanikisha azma ya ulipaji kodi katika nchi yao.
Aidha maesema licha ya kuendelea kutoa elimu pia watatumia vyema teknolojia katika  kukusanya mapato ili kuepuka mapato yanayokusanywa kupotea.
Mkutano huo wa 44 uliofanyika katika ukumbi wa Bank kuu Tanzania kinazini mjini zanzibar umeshirikisha Makamishna wa Nchi 6 ikiwemo Tanzania ,Uganda,Burundi ,Kenya ,Ruwanda na Sudan na umejadili mambo mbalimbali juu ya ukusanyaji wa mapato nchini ikiwemo kuzuia mianya ya rusha katika kukusanya mapata.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI