Kampuni ya StarMedia rasmi imezindua kuonyesha mechi 64 za Kombe la Dunia, michuano itakayofanyika nchini Russia na kuwatangaza mabalozi wake.
Mabalozi hao wataiwakilisha StarTimes wakati wa michuano hiyo itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Russia.
Kazi ya mabalozi hao wakiwemo wasanii wa muziki, uigizaji na wanasoka, wamepata king'amuzi kila mmoja ili kuendelea pia kufaidi michuano hiyo na wao wakiendelea kujifunza ubora wa ving'amuzi hivyo.
Michuano hiyo itaanza Juni 14 nchini Russia na mechi zote 64 zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes kilicho chini ya kampuni ya StarMedia.
Mabalozi wametangazwa akiwemo msanii maarufu Wema Sepetu, pamoja na wasanii wengine maarufu kama Hamad Ally maarufu kama Madee, mchekeshaji Mkude Simba, msanii Man Fongo, Mkali Wao, Ibitoke, mwigizaji Monalisa, Mkude Simba na wengine ambao watafanya kazi ya ubalozi.