Hata mfumo wa timu ubadilike Vipi lakini kuna nafasi mara nyingi kuna nafasi hazibadikiki sana au hazibadiliki kabisa. Nafasi ya mlinda lango na kiungo mkabaji. Wapo baadhi ya makocha wao hawaamini sana katika nafasi ya kiungo mkabaji (Pep Guardiola)
Vikosi viwili vya mabingwa wa miaka miwili iliyopita vilitengenezwa kwa kuunganishwa na N’golo Kante. Katika nafasi hii Guardiola ametengeneza uhusiano mzuri wa wachezaji wawili kwenye kundi la viungo watano kama sehemu ya kazi aliyokuwa akifanya Kante. Viungo David Silva na Kevin De Bruyne wamemzunguka Fernandinho kufanya kazi yake kuwa rahisi. Hii ni tofauti kidogo kwa Man United ambayo Nemanja Matic ndiye mhusika lakini amezungukwa na viungo wa kariba yake (Herrera, Pogba, Mctomney) wote hawa wametumika kucheza nafasi ya Kante.
Mabingwa wa ulaya Real Madrid wao wana Casemiro, ambaye huenda akatumika kwenye nafasi hiyo hata kwenye timu ya taifa kuliko Fernandinho.
Kiungo huyu lazima awe na uhakika wa kucheza dakika 90.
Leicester’s walijaribu kuziba pengo la Kante kwa kumnunua Wilfred Ndidi. Msimu huu Ndidi ndani ya dakika 90 amenyang’anya mpira kwa aina ya kutelezea kwa mpinzani (sliding tackles) mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote yule. Rekodi hii iliwekwa na Kante msimu wa mwaka 2015/16.
Joe Allen ameshindwa kabisa kukamilisha kazi aliyotumwa Stoke lakini bado yupo kwenye orodha ya Viungo waliocheza tackling au Manowari nyingi.
Kiungo mwenye kazi ya kipkee uwanjani Oriol Romeu anayekipiga Southampton ameonesha uwezo wa yake msimu kwenye eneo la katikati. Romeu amepata msaada mkubwa kutoka kwa kijana wa kispanyola Mario Lemina . Romeu amefanya manowari 3.4 kila mara timu yake ilipokuwa haina mpira. Kiungo wa
Huddersfield Aaron Mooy hayupo mbali sana akiwa na wastani w manowari 3.3, na kila monawari aliyocheza anawastani wa rafu (4.5), huku kante akimfuata kwa karibu 3.3.
Huddersfield Aaron Mooy hayupo mbali sana akiwa na wastani w manowari 3.3, na kila monawari aliyocheza anawastani wa rafu (4.5), huku kante akimfuata kwa karibu 3.3.
Emre Can ana wastani wa 81.3 %, kwa manowari zilizokamilika mjerumani huyu anafuatana kwa karibu kwenye Manowari zilizokamilila bila rafu akiwa na Kante na Jonathan Hogg. Mooy anakosea nidhamu nzuri ya kucheza manowari bila kusababisha faulo.
Jitihada za Idrissa Gueye kutoka upande wa Mersey. Mwamba huyu kutoka Senegal. Ni mchezaji namba mbili kwa kucheza manowari nyingi, ni mchezaji namba mbili ambaye manowari zake zimekamilika kwa wingi (kupokonya mpira), ni mchezaji namba 3 ambaye ana wastani wa kucheza manowari bila rafu.