TIMU ya Arsenal inaweza kumkosa mshambuliaji wake, Alexandre Lacazette kwa wiki sita baada ya Mfaransa huyo kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kushoto.
Klabu imethibitisha Lacazette aliumia goti na kufanyiwa upasuaji jana asubuhi na atakuwa nje kwa wiki sita baada ya zoezi hilo.
Arsenal imesema upasuaji wa goti hilo umetokana na tatizo dogo, lakini Lacazette atapatiwa tiba zaidi.
Lacazette
alipoteza nafasi mbili nzuri za kusawazisha Jumamosi Arsenal ikifungwa
1-0 na mahasimu wao wa London, Tottenham baada ya kuingia akitokea
benchi.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexandre Lacazette atakuwa nje kwa wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Mfaransa
huyo alijiunga na klabu kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 52, lakini
rekodi yake ilivunjwal na Pierre-Emerick Aubameyang aliyewasili Arsenal
kwa dau la Pauni Milioni 56.
Lacazette
alitarajiwa kuingoza safu ya ushambuliani ya Arsenal katika mechi ya
Europa League dhidi ya wenyeji, Ostersunds FK, lakini maumivu
yanamuondoa.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Lyon atakosekana pia kwenye fainali ya Carabao Cup
dhidi ya Manchester City Uwanja wa Wembley on February 25.
Lacazette
alikuwa ana mwanzo mzuri Emirates akifunga mabao manne katika mechi
sita za kwanza tangu asajiliwe kuroka Ufaransa, lakini tangu hapo
amefunga bao moja tu kati ya 13.
MECHI AMBAZO ARSENAL ZITAMKOSA ALEXANDRE LACAZETTE
Februari 15 – Ostersunds (away) – Europa League last-32
Februari 22 – Ostersunds (home) – Europa League last-32
Februari 25 – Man City (Wembley) – Carabao Cup final
Machi 1 – Man City (home)
Machi 4 – Brighton (away)
Machi 11 – Watford (home)
Machi 17 – Leicester (away)