Mkuu wa hifadhi ya Taifa Jozani Ali Mwinyi Anaeleza kuwa moto huo unakadiriwa kuwa umeanzushwa na ulimaji waAsali, na juhudi za kuzima moto huo zimefanikiwa baada ya kuitana na jamii napia kuchukua juhudi ya kuwaita zimamoto katika kituo cha kitogani.
Amesema kuwa takriban kila mwaka kunakuwa kuna tokezea tukio kamahilo la moto wa kushtukiza.
Kwahiyo amewashauri wale ambao wana lima Asal kutochoma moto ovyo walime asali kwa njia za usalama.
Baadhi ya wananchi wanaokaa katika eneohilo wametoa wito kwa wanaoutumia msitu huo kwa kulimia asali kutochoma moto ovyo ili na kutumia uangalifu zaidi katika kazi zao.
Moto huo umeanza kuwaka ndani ya tarehe 17 ya mwezi huu na hadi sasa jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea ambapo zaidi ya hekta 19 zinakadiriwa kuteketea.