Wakati Simba
imetuma mtu mapema kwenda Djibouti kwa ajili ya maandalizi ya mechi ijayo dhidi
ya Gendamarie, wanaotarajiwa kuwa wapinzani wao wameonyesha nao wako makini
zaidi.
Al Masry ya Misri
wanajipa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho dhidi ya
Buffaloes ya Zambia baada ya kushinda kwa mabao 4-0 mechi ya kwanza.
Kutokana na hivyo,
wametuma mmoja wa watu wa ufundi kutoka katika benchi lao kuangalia uchezaji wa
Simba, hasa inapokuwa ugenini.
“Tayari kuna mtu
ameandaliwa kwenda Djibouti kuangalia mechi ya mwisho ya Simba. Hata kama
itakuwa nyepesi lakini watapata uhakika namna ya mchezo wao.
“Wanafanya mambo
mawili kwa wakati mmoja, hapo wanajiandaa na mechi ya pili huko Zambia. Wana
asilimia themanini ya kuvuka. Hapo hapo wameanza kujiandaa na Simba,” alisema
Mtanzania anayeishi nchini baada ya kuzungumza na SALEHJEMBE.
Iwapo Simba itavuka, basi ina nafasi kubwa ya kukutana na Al Masry ambayo inaonekana Simba watalazimika kufanya maandalizi ya uhakika hasa.