Kwa rekodi zinaonesha Manchester United wanakwenda katika mchezo wa leo wakiwa kama wanyonge wa Chelsea, Chelsea ni kati ya vilabu ambavyo vimekuwa vikiwaonea sana Manchester United.
Katika michezo 14 iliyopita baina ya vilabu hivi viwili, Manchester United wamepata ushindi mara moja tu na ilikuwa kombe la ligi msimu uliopita huku wakipigwa michezo nane na kupata suluhu mitano.
Pamoja na unyonge wa United lakini wamekuwa wagumu sana katika uwanja wao wa nyumbani haswa katika ligi ya EPL kwani mara ya mwisho Chelsea kupata bao Old Traford katika mechi za EPL ilikuwa October 2014 bao la Didier Drogba.
Na pia kwa rekodi ni ngumu kuwapa Chelsea ushindi kwani katika mchezo baina ya timu hizi mbili hakuna timu ambayo imepata ushindi ugenini tangu Chelsea walipowafunga Manchester United bao 1 kwa nunge mwaka 2013.
Katika kuonesha kwamba Chelsea ni wababe wa United, United wameruhusu nyavu zao kuguswa na Chelsea mara 67 katika mechi 18 walizopoteza kwa Chelsea na hii ni idadi kubwa zaidi kwa United kufungwa na timu nyingine.
Katika michezo 49 ambayo Jose Mourinho amecheza katika uwanja wa Old Traford amepoteza michezo miwili tu na michezo hii miwili yote alipoteza dhidi ya wapinzani wake wakubwa Manchester City.
Chelsea nao katika michezo yao tisa iliyopita katika mashindano yote wamefanikiwa kupata ushindi mara mbili tu na wakapata suluhu nne na kupoteza michezo mitatu rekodi ambayo sii nzuri sana kwa Conte ugenini.