Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jioni hii na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, na Viongozi wengini wa Mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika Uwana wa Ndege Mwanza kuaza ziara yake ya Kiserikali Mkoani humo.
Makamu
wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika Uwana
wa Ndege Mwanza kuaza ziara yake ya Kiserikali Mkoani humo.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo
itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018,
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli
na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine
ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami
Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za
Mjini.
Makamu wa Rais
atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi
siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya
(Meatu)
Tarehe 21, Makamu
wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda
Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na
kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji la Samia Suluhu Hassan
katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika
viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .