Mambo
yanabadilika kwa kasi kubwa na huenda itakuwa ni vigumu sana kuyazuia
mabadiliko hasa katika klabu kongwe kama Yanga na Simba.
Simba wameanza na watani wao, Yanga nao wanaonekana wako njiani.
Kwani
Kamati ya Mabadiliko ya Mfumo wa Uendeshaji wa Klabu ya Yanga chini ya
mwenyekiti wake, Wakili, Alex Mgongolwa kukutana kwa ajili ya kufikia
muafaka.
Unaweza
kusema ni neema inakaribia Yanga kwani mara baada ya kamati hiyo
kukutana itapeleka ripoti kwenye Kamati ya Utendaji ya timu hiyo
itakayotoa majibu kipi kifanyike.
Yanga
wanataka kuleta mabadiliko hayo, ikiwa ni siku chache Simba kubadili
mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo kwa kumuuzia hisa mfanyabiashara
maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Taarifa zinaeleza kamati hiyo ilikutana juzi Jumatatu usiku na kujadili mfumo wa mabadiliko hayo ya Klabu ya Yanga.
“Kamati
yetu mpya tuliyoiteua ya Mabadiliko ya Uendeshaji wa klabu ilikutana
juzi Jumatatu usiku na kikubwa ilikuwa makubaliano ya jinsi ya kuendesha
klabu yetu ambayo inaturuhusu kikatiba.
“Na
mifumo iliyopangwa kujadiliwa ni mfumo upi sahihi kati ya kampuni au
kuuza hisa kwa muwekezaji kama ilivyokuwa kwa watani wetu wa jadi
Simba.”
Alipotafutwa
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia suala hilo, alisema:
“Ni kweli kabisa kamati hiyo ilikutana lakini nisingependa kuweka wazi
kila kitu hivi sasa.”
Wajumbe
wengine wanaounda kamati hiyo ya mfumo mpya wa mabadiliko ni Said Mecky
Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed
Nyengi.