Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude
ameutaka uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuongeza umakini
katika hatua ya lala salama ya Ligi Kuu Bara ili kuepukana na vitendo
vya hujuma ambavyo vinajitokeza.
Mkude ametamka hayo baada ya kudai kuwa
kuna njama ambazo zinafanyika na wapinzani wao katika ligi kuwaumiza
baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kuwapunguza kasi.
"Binafsi namkubali sana Bocco na
anapokosekana katika kikosi chetu huwa sijisikii vizuri kwani ni mmoja
kati ya washambuliaji wakuigwa hapa nchini."
“Ni mpambanaji na haogopi kuumia
anapokuwa akipambana kuitafutia ushindi timu yetu, lakini kuna mchezo
mchafu ambao umeanza kufanyika wa kutaka kumuumiza makusudi ili tu
kuipunguza makali timu yetu, hiyo siyo sawa TFF wanatakiwa kuwa makini
katika hilo,” alisema Mkude baada ya Bocco kuumizwa katika mechi ya ligi
dhidi ya Mwadui FC.
HABARI KUU